Thursday 29 October 2015

NANI NYUMA YA PAZIA LA KURA FEKI KATIKA UCHAGUZI MKUU 2015??????


Ukijiuliza utapata majibu. Nani amekuwa nyuma ya kura fake ambazo zimekuwa zikikamatwa kipindi cha uchaguzi? Je Usalama wa Taifa hawajui kabisa ni nani ambaye amehusika na "USHENZI" huo? Hivi Rais Kikwete hajui lolote kuhusu kura hizo ambazo zote zilizokamatwa zimeonekana kumpigia Pombe Magufuli? Tukisema kuwa Serikali ya Kikwete ndiyo imehusika na ushetani huo tutakuwa tumekosea wapi? Ni kura ngapi ambazo zilifanikiwa kuingia kwenye masanduku na hivyo kuwakosesha wananchi haki yao ya kidemokrasia? Kama Serikali hii haihusiki mbona iko kimya kwenye kukanusha hilo?

Mwanafunzi mwenye uhakika na somo analokwenda kufanyia mtihani huwa haingii kwenye chumba cha mtihani akiwa na "majibu fake"! Viongozi fake watazidi kulifanya Taifa letu liwe fake na kuzidi kudharauliwa na mataifa mengine jirani. Tuna kila rasilimali ya kutupa mafanikio lakini kwa kuwa watawala hawana "akili sahihi" ndiyo maana tunazidi kushindwa kama Taifa katika mitihani ya maisha. Nawaza ni nani aliyekuwa nyuma ya kura fake? Je, kweli tumekuwa na uchaguzi huru na wa haki?

                                                  BY WAZOHURU.COM

No comments:

Post a Comment