Wednesday 20 April 2016

BIASHARA NDOGONDOGO ZENYE FAIDA KUBWA

Kila Biashara inaweza kuwa endelevu.., Wachina wana msemo hata safari ndefu inaanzia kwa hatua moja.

Kwa maana hiyo tafuta chochote kinachoweza kununulika sehemu ulipo kwa bei nafuu na uza kwa bei yenye faida kidogo, baadhi ya hivyo ni:-

  • Kukata matunda kuweka kwenye containers na kuuza
  • Kuuza voucher pamoja na vingine vidogo vidogo (nunua vitu vya jumla uza reja reja)
  • Pita kwenye mahoteli na migahawa chukua tender nenda nje ya mji nunua kuku, samaki, mboga mboga n.k. uzia hizi hoteli na migahawa kwa faida ndogo
  • Uza magazeti (hii huitaji mtaji) nenda kwa
    wakala atakupa magazeti, ukiuza faida yako, yakibaki unarudisha, (hakuna hasara)
  • Nunua Boda boda endesha mwenyewe au kama kuna kijana muaminifu akuendeshee
  • Nenda kwa wanaofungua robota za mitumba chagua nguo nzuri nzuri zifue na zipige pasi utembeze maofisini

Utaona kwamba vitu vya kufanya ni vingi issue ni kwamba location yako kuna mahitaji yapi na wewe upo tayari kufanya kipi, kumbuka sio kila anachokifanya huyu..., yule anaweza kukifanya hulka za watu na salesmanship zipo tofauti fanya kile ambacho wewe upo comfortable na kwenye vyote fanya SWOT analysis uone kipi kitakufaa wewe, usiige kwamba fulani kafanya kafanikiwa ukadhani ni given na wewe ufanikiwa,

MUHIMU KWA WANAOTAKA KUPATA TENDA MAHOTELINI,Zingatia
Hoteli kubwa yoyote wanachoangalia zaidi ya lolote ni guarantee ya wewe kuweza ku-deliver., jambo ambalo linawashinda wengi, sababu wakikwambia tunataka mayai kadhaa kwa siku hawategemei kesho yaje uwapigie simu sijui kuku wamekufa au leo nimepata nusu...

Ndio maana watanzania wengi wanashindwa hata kupata tender sehemu kama migodini, na wenzetu wakenya ni wajanja wana-form Ushirika na wanaomba na kuuza mayai yao kwa pamoja.., sababu hapo wanakuwa na guarantee wa kuweza kupata idadi yoyote ya mayai siku yoyote. Kwahio kama kwenye hoteli kubwa ukiweka contract ya kuwapelekea mayai 500 kila wiki lazima upeleke hayo 500..., ndio maana nikasema huenda kwenye hoteli ndogo, ndogo au migahawa ila kama unao uwezo wa kukidhi deliver ya mayai kiasi fulani bila kukosa nenda to kwenye mahoteli ongea na watu wa manunuzi kama bei yako ni product yako ni safi sioni kwanini wasikupe tender..

Kama huwezi ku-guarantee kiasi fulani cha mayai basi ungana na wafugaji wenzako huko Morogoro tengenezeni ushirika na muuze kwa pamoja.., yaani kila mfugaji chochote anachokipata anapeleka kwenye ushirika alafu huo ushirika ndio unatafuta tender. Na hii itasaidia hata kununua vyakula mkinunua kwa pamoja mnaweza mka-bargain bei.
USHAURI
Kila biashara inalipa apa Tanzania cha msingi uipende, uijue, uwe na muda wa kutosha wa kusimamia. ila nakuomba usifanye biashara yoyote iliyo kinyume na sheria za nchi. unaweza faida yake ukaimalizia jela. fanya biashara inayokubalika mbele ya jamii na mbele za mwenyezi Mungu. utaziona Baraka zinakuwa nyingi mkuu.

No comments:

Post a Comment