Aina za bustani
1. Unawezatumia makopo amabayo mala nyingi hutumika kupata maua kando kando ya nyumba
2. Unaweza tumia gunia la kubwa..
3. Unaweza tengeneza key hole garden ( bustani ya tundu la Ufunguo)
BUSTANI YA MAKOPO/NDOO
Vifaa
Udongo, makopo/ndoo, mchanga/Pumba za mpunga (Rice husk), Mbole ya samadi iliooza vizuri.
Udongo - Kwa ajili ya kuwezesha mmea kusimama, pia kupatia virutubisho mmea
Mchanga/Rice husk - Kusaidia mizizi kupita kwa urahisi, pia kuweka
mazingira mazuri ya hewa na maji katika udongo yaani mzunguko wa maji na
hewa.
Mbolea ya samadi - Kutoa virutubisho kwa mmea
Hatua za utengenezaji.
- Changanya udongo wako na mchanga/rice husk pamoja na mbole katika uwiano wa 5:2:1.
5 udongo, 2 samadi, 1 Mchanga/rice husk
- Toboa makopo yako kwa chini ili kuzuia maji kubaki kwa wingi kwenye kupo na weka pamba kwenye matundu uliotoboa.
- Weka udongo uliochanganywa vizur kwenye makapo/ndoo. Hapo utakuwa tayar kupanda mbegu zako ama mche wa mboga aina yoyote.
- Kuepuka uchafuzi wa mazingira kwa maji yanayo toka kwenye makopo
endapo makopo hayo yapo kwene simenti, weka makopo/ndoo hayo juu
sahani/beseni.
Uangalizi.
- Mwagilia mboga yako mala baada tu ya kupanda na kuendelea ikitegemeana ni aina gani ya mboga.
- Unapoona magonjwa hasa fangasi wa ukungu na wadudu wa mboga unaweza
tumia dawa zisizo za kikemikali za viwandani kama vile majani ya
pilipili kichaa, mwarobaini na tumbaku.
- Mboga kama sukuma wiki waweza vuna mara kwa mara, kazi yako ni kumwagilia tu.
- unatakiwa kubadilisha udongo wako kwa muda mfano. baada ya mavuno 2
ili kuakikisha mboga zako zina pata virutubisho ya kutosha.. ( Hii
inategemeana ni aina gani ya mboga)
Faidi
- Inapunguza utumiaji wa kemikali za viwandani
- Gharama za uhitaji wa mboga za majani
No comments:
Post a Comment