Inachukua siku 60 tu kuvuna tangu plus siku 3-5 za kukaa ardhini, kwa hiyo kwa mwaka nalima mara 4 tu nina ekari 5 na kila eka napata kuanzia 2M-3M.
Spacing ni 2mx2m na kila shimo naweka mbegu 2 ambazo zinazaa matunda 2-3 kwa maana kila shimo napata matunda 4-6 ( wastani matunda 5).
Hivyo kwa spacing hiyo napata mashimo 1000-1200
Idadi ya matunda: Mashimo x Matunda kwa shimo x ekari [1,000 x 5 x 5 = 25,000]
Mapato: wastani wa shilingi 500 kwa tikiti x idadi ya matikiti kwa eneo la ekari 5 [25,000 x 500 = 12,500,000]
Mapato kwa mwaka: 12,500,000 x 4= 50,000,000
Gharama za uendeshaji wa shamba ni Tsh 25,000,000
Faida Kuu ni Tshs 25,000,000
Ushauri: Kwa mafanikio mazuri na kuinuana kiuchumi wakulima wakiungana na kufanya kilimo bishara watakuwa na nafasi kubwa ya mafanikio kwa maana kiuchumi wanataweza kusaidiana ili kuinua mtaji na kuweza kupata kiasi cha kuanzia shughuli zao za kilimo.
Ili kulima matikiti maji, inakubidi uwe na sehemu ya
kutosha, yenye jua la kutosha, maji mengi na ardhi yenye rutuba ya kutosha,
matikiti maji hukua haraka kama mimea mimgine ya jamii yake itambaayo mfano
Matango, maboga na maskwash.
Kwa mtu ambaye anaanza kilimo yatampa tabu kidogo tofauti na
Yule ambaye ana ujuzi kidogo na mambo ya kilimo kwa sababu yanahitaji umakini
kiasi.
HALI YA HEWA
Mimea hii haihimili hali ya joto kali sana, mvua nyingi na
udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu, inastawi
vizuri kwenye kuanda wa pwani na miinuko kidogo kama DSM,Tanga, Morogoro,
Mtwara, lindi na Pwani ambapo kuna jua la kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni
kipindi cha kipupwe mwezi wa machi mpaka wa septemba .
UPANDAJI
Panda kwa kutumia Mbegu zinazouzwa madukani, ukitumia Mbegu
kutoka kwenye tikiti ulilonunua linaweza likawa ni hybrid na matokeo yake
matikiti yatakayozaliwa hayatakuwa bora kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili
(F2)
Panda Mbegu yako moja kwa moja kwenye shamba, usinunue miche
au kupanda Mbegu kwenyemifuko ya plastiki halafu ndi uhamishie shambani, panda
Mbegu mbili sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa sentimeta 30 kutoka shina
hadi shina na mita 2 - 3 kutoka mstari hadi mstari, baada ya siku chache Mbegu
zitaanza kuota, baada ya kama wiki 2 katika Mbegu mbili ulizopanda kata moja na
uache ule mche wenye afya zaidi, angalizo using’oe mche bali ukate ili kuzuia
kusumbua mizizi ya mche uliobaki.
Unaweza kupandishia udongo kwenye mashina na hii itasaidia kupunguza
maji yasituame kwenye mimea yako, pia unaweza kuweka samadi badala ya
kupandishia udongo ukiwa na nia ileile ya kuzuia maji yasituame na kuongeza
rutuba.
Kama una sehemu ndogo ya shamba unaweza kuyawekea matikiti
waya wa kutambalia, ila inabidi uwe imara kwa sababu ya kuhimili uzito wa
matunda yenye, na wakati wa kuanza kutambaa kwenye waya ni lazima uifundishe
mimea kwa kuielekezea kwenye waya na kufungia
MCHE ULIOCHIPUA
UANGALIZI
Miche ikiwa imetambaa kiasi unaweza kuweka matandazo kwenye
udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu, unaweza kuweka samadi au mbolea za
viwandani, mimea ikiwa midogo tumia zaidi mbolea zenye nitrojen na utumie zaidi
mbolea za potasiam mara baada ya maua kutokeza hadi matunda kukomaa, matawi
yakifikia urefu wa mita 2 kata mbele ilikuruhusu kutoa matawi na hivyo kupata
maua mengi zaidi hatimaye mavuno zaidi
MAUA NA MATUNDA
Matikiti hutoa maua dume na jike kwenye tawi moja, maua dume
ambayo ni madogo zadi hutoka kwanza yakifuatiwa na maua jike ambayo ni makubwa
zaidi, usipoona maua dume na jike kuna tatizo mfano maji kidogo yalimwagiliwa,
upungufu wa viritubisho kwenye udongo, hali ya hewa ni joto/baridi sana n.k
Uchavushaji kwenye matikiti hufanyika na wadudu, kama
huwaoni wakifanya kazi yao unaweza kufanya mwenyewe, muda mzuri ni wa asubuhi,
unakata maua dume kwa kisu na kufanya uchavushaji kwenye maua jike, maua jike
ya mwanzo kwenye tawi ndiyo yenye ukuaji bora zaidi, unaweza kukata tawi
lisiendelee kukua baada ya matunda kutokeza hii husababisha kuwa na matunda
makubwa zaidi
UCHAVUSHAJI KWA MKONO
UVUNAJI MATIKITI
Ili kujua matikiti yamekomaa inahitaji ujuzi kidogo, upande
wa chini wa tunda huanza kuwa na rangi ya njano, pia kikonyo juu ya tunda
hukauka kabisa na kuwa kijivu, ila njia nzuri ni kuyapiga kwa kiganja na kusikiliza
mlio wake kama tunavyofanya kwenye mafenesi, hii nayo ni shule nyingine. Tumia
kisu wakati wa kuvuna matikiti, yabebwe na kuhifadhiwa vizuri kwenye makasha
tayari kuuzwa au kwa matumizi binafsi
MAGONJWA NA WADUDU
Wadudu wa matikiti wako wanaoshambulia majani na maua, na
wengine hushambulia matunda , pia kuna magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia
mimea, ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo
kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kjupata dawa sahii, dawa aina ya
KARATE itasaidia kuua wadudu wa majani, maua na matunda na FUNGICIDE itasaidia
kwa mashambulizi ya fangasi
Posted by Bennet at 17:59 @ http://mitiki.blogspot.com
No comments:
Post a Comment