ZINGATIA:
Tukumbuke idadi kubwa ya vijana wameonesha hamasa kubwa katika zoezi zima la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.Wakiwa na matamanio makubwa ya siku ya upigaji kura kumchagua RAIS, MBUNGE NA DIWANI. wengi wetu wakiwa na fikra za MABADILIKO. JE? MABADILIKO haya yatawezekana pasipo kuhakikisha unapiga kura katika hali ya nidhamu na kufuata taratibu zote za upigaji wa kura! Ushindi wa mabadiliko umeshaonesha mwangaza, hivyo basi pasipo kufifisha mwangaza na nuru ya ukombozi ilioletwa na MH EDWARD LOWASSA, hatuna budi kuwapa elimu vijana juu ya nidhamu, taratibu na sheria za upigaji kura kwani wengi wao ni mara yao ya kwaanza kuingia kwenye chumba cha upigaj kura. Fomu za mifano zitumike kuwafikia na kufundishia vijana juu ya namna sahihi ya kukitumia kikatio chako! Kura ni HAKI YAKO YA MSINGI. KURA VYAKO MOJA INAWEZA KUYABADILISHA MATOKEO YA UCHAGUZI.ITUMIE VIZURI NAFASI HIYO KUWAWAKILISHA WATOTO NA WENGINE WASIONA SIFA ZA KUPIGA KURA. Kuzingatiwa kwa hili CHADEMA watakua wamejihakikishia ushindi mnono pasi na shaka.
(MUHIMU)
Baada ya kuweka tiki kwa
mgombea wako uliempigia kura hakikisha hauchafui karatasi ya kupigia
kura kwa kuichora au kuandika kitu chochote kwani kwa kufanya hivo
utakuwa umeharibu kura yako na utakuwa umejikosesha haki yako ya msingi
MAMBO YA KUYAEPUKA SIKU YA KUPIGA KURA
1-Baada ya kumaliza kupiga kura toka nje bila kubuguzi watu wengine wanaohitaj kupiga kura kama ulivofanya wewe
2-Hakikisha hauvai sare ya chama
chochote huenda ikawa ni Chadema, Cuf, Ccm, Act maana kwa kufanya hivo
kutaweza kusababisha usipige kura yako na ukawa umejikosesha haki yako
ya msingi.
3-Epuka kuweka vikundi katika maeneo ya kupiga kura yenye lengo la kuhamasisha wananchi wenzio wampigie kura mgombea gani.
4-Hakikisha baada ya kupiga kura unakaa mita 200 kutoka eneo ulilopigia kura ili kusubiria matokeo ya uchaguzi uliofanya.
No comments:
Post a Comment