BY BBC SWAHILI<<<<CLICK FOR MORE INFO>>>
Mgombea wa urais kupitia tiketi ya
chama cha CHADEMA Edward Lowassa amesema kuwa hatokubali matokeo ya
uchaguzi wa urais yanayoendelea kutolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
nchini Tanzania (NEC).
Kiongozi huyo amesema kuwa ana ushahidi wa kutosha kwamba kuna udanganyifu uliofanyika.
Amesema kuwa kura za chama hicho zimepunguzwa katika vituo vingi vya kupigia kura.
Akihutubia
wanahabari pamoja na viongozi wengine wa upinzani, amesema kwamba kura
zilizohesabiwa katika maeneo tofauti haziambatani na matokeo
yaliyotolewa.
Lowassa ameongezea kwamba maeneo yote ambayo
walipata ushindi yamecheleweshwa. Aidha, amelalamikia kukamatwa kwa
maajenti wa chama hicho akidai kuwa ni ishara za kutaka kuiba kura.
No comments:
Post a Comment