Watu wamejitokeza kwa wingi katika
uchaguzi wa Tanzania unaotajwa kuwa na ushindani mkubwa huku muungano
mpya wa upinzani ukijaribu kukiondoa madarakani chama tawala CCM
kilichoshikilia madaraka kwa miaka 54.
Katika maeneo mengine ,upigaji kura uliongezewa mda ili kuwapatia fursa wale walio katika milolongo mirefu kupiga kura.Kura ya maoni imekiweka chama tawala cha CCM kifua mbele lakini matokeo hayo yanatarajiwa kuwa ya ushindani mkubwa.
Vyama vinne vya upinzani vinamuunga mkono mgombea mmoja ,aliyekuwa waziri mkuu.
Kujitokeza kwa wingi kwa raia ili kushiriki katika uchaguzi huo kunamaanisha kwamba Watanzania wanaamini kwamba uamuzi wa maisha yao ya baadaye uko mikononi mwao.
Hi ni tofauti na uchaguzi mingine iliopita ambapo CCM ilitarajia ushindi kutokana na upinzani uliodhoofika na kugawanyika.
Lakini siasa zimebadilika nchini humo kufutia kubuniwa kwa muungano wa Ukawa ambao unaamini una fursa kubwa ya kuibuka mshindi.
Rais Jakaya Kikwete ambaye anaondoka madarakani ametaka kuwepo kwa amani wakati na hata baada ya uchaguzi,huku akionya kwamba mtu yeyote atakayejaribu kuathiri amani ataadhibiwa vilivyo.
Katika eneo la kimara ambapo wapiga kura waliyachoma makaratasi ya kupigia kura,maafisa wa uchaguzi wamerudi na sasa raia wanatarajiwa kupiga kura.
No comments:
Post a Comment