Saturday 5 September 2015

MBINU KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO BAADA YA KUHITIMU SHAHADA YA KWANZA.


Umefanikiwa kuikamilisha safari ya kuelekea  ulimwengu wa wasomi (cheti cha shadaha ya kwanza). Tamaa ya mafanikio na kujitegemea vinakuingia, kama ukiwa mpenda maendeleo wa kweli aliye na”uchu” wa mafanikio kama kijana (taifa la leo).  (swali) “je unaweza vp kupambana na ulimwengu wa watafutaji?
Nitatafuta kazi!!!....hili ni jibu sahihi utakalolipata kutoka kwa kila muhitimu.
Je? Unapaswa kufanya nini ili upate iyo kazi?
Miongoni mwa majibu apo chini.

ANDAA CV NZURI
JIWEKE TAYARI KWA USAHILI (INTERVIEWS)
ANZA KUTAFUTA KAZI.
Kufikia hapo itakua tayari umeshagundua hitaji la kukuza taaluma yako kwa nadharia (practical). Hili ni suala la kwanza na kawaida kwa kila mhitimu kulifikiria.
Zingatia haya.
 I. Katika kampeni zako za utafutaji kazi, usisite kuhudhuria katika semina mbalimbali unazoamini zinaweza kukuonesha fursa kadha wa kadha za ajira.
ii. Pia katika makungamano ya wasomi elimu ya juu, hapa utapata fursa ya kukutana na kubadilishana mawazo na wasomi wenzako sambamba na kukuza upeo wako wa uelewa kuhusiana na mambo mbalimbali ndani na nje na nchi. iii. Bila kusisahau kuhudhuria katika tovuti mbalimbali zinazotoa matangazo ya ajira.
Kwa msaada: follow links below

www.jobstanzania.net
www.zoomtanzania.com
www.ajira.info
www.ajiraonline.com
www.kazibongo.blogspot.com
www.jobs.co.tz
www.nafasizaajira.com
www.ajirakwanza.com
www.vijanatz.com/tz/jobs
www.ajira.go.tz

Ni wazo zuri sana kama utajitahidi kua karibu na wahitimu wenzako uliomaliza nao elimu ya juu. Huwezi jua labda unaweza ukapata taarifa za fursa nyingine ambazo pengine isingekua rahisi kukufikia. Hapo utapata mawazo mapya na mbinu za kukabiliana na ugumu wa maisha pia.
Kwa wale waliofaidika na mkopo wa elimu ya juu (heslb) wasisahau kwamba huu ndio muda muafaka wa kulipa fedha izo. (dawa ya deni kulipa)
Kama uliweza kuthubutu kupambana na umefanikiwa kuipata shahada ya kwanza uliyoitesekea kwa muda usiopungua miaka mitatu (3), bila ya kujali vikwazo vingi ulivyopitia. Huu ni muda wa kula matunda ya mazao uliyoyapanda.

Haya ni mambo machache ya kuzingatia kabla hujafanya maamuzi ya namna ya kuitumia shahada yako.
IMARISHA UJUZI NA TAALUMA YAKO.
 Uliweza kuyamudu maisha  na mpaka kuthubutu kuongeza ujuzi kwa kipindi chote ulichokua chuoni.
Sasa ni muda wa kuanza safari ya kuimarisha na kukuza fani uliyoisomea. Zipo njia kuu mbili kuelekea kilele cha safari yako. Ya kwanza ni ajira, na ya pili ni ujasiriamali. Ambapo limefanywa kama ni moja ya somo miongoni mwa masomo thelathini na saba (37) niliyowahi kusoma tangu nimeanza elimu ya msingi.
ANDAA CV YAKO
Hatua ya pili ni kutafuta mahala unapoweza kupata msaada wa kukamilisha maandalizi ya cv yako. Yapo maduka mengi sana ya vifaa vya maofisini maarufu kama (stationary) na hapa ndio mahala sahihi kwa maandalizi yako ukiwa na msaada wa mtu mzoefu katika masuala ya kuandaa cv iliyo bora.
Cv ni hadithi kuhusiana na historia yako kwa ufupi kitaaluma. Uzuri wa ubora wa hadithi hii ndio utakaokutetea kuweza kuipata kazi unayoitamani (dream job) kwa maisha yako ya sasa na ya baadae.
Siri ya cv inayoweza kumshawishi afisa wa ajira ni ile iliyo jikita katika
·         Ubora (strong)
·         Inayoelezeka kwa urahisi (clear)
·         Yenye upekee na ushawishi  machoni mwa kila mwajiri (exciting)

VIDOKEZO VYA KUIBUKA KIDEDEA KATIKA USAHILI.
Umeshaipata shahada ya kwanza, ushaandaa cv yenye ubora wa kuhamasisha, na hatua inayofuata ni kutafuta kazi.je? Utaweza vipi kutetea ubora wa cv yako kwa maafisa waajiri! Hili ni swali lisilo na majibu kwa wahitimu tulio wengi.
Usahili wa kazi (job interview) ni mahojiano ya kina na ufupi kulingana na cv yako inavyojieleza (hadithi ya masha yako halisi). Usifanye makosa, uwezo wa kumudu usahili kwa kutoa maelezo yenye lishe na nakshinakshi za ubora ndani yake ndio utakao kupa matokeo chanya ya kampeni za kupata kazi ya uwakika yenye kukidhi mahitaji yako. No pressure!

Siri tatu za usahili utakaoweza kumshawishi afisa mwajiri.
  •  jiandae kikamilifu
  •  vaa uhalisi
  •  jiamini
Hizi ndizo miongoni mwa siri kuu 3 zinazozingatiwa na maafisa waajiri katika usahili wa wafanyakazi wapya.

No comments:

Post a Comment