Kuingia uraiani baada ya kumaliza masomo ya elimu ya juu Ni
suala lenye uzito wake kwa idadi kubwa ya wanafunzi vyuoni. Kufanyia kazi
masomo uliyosomea darasani kwa nadharia. Pasipo muda wa kukusubiri, shinikizo
la bosi na changamoto nyingi zilizopo maofisini. Pia ni muda huu tunapokosa
uhuru wa kujipangia ratiba zetu binafsi.
Siri ya kufanya maisha yako yasiwe ya upweke na msongo wa
mawazo juu ya ntapata wapi kazi, au ntafanya nini ili niweze kupata kipato
baada ya kumaliza masomo yako ni kuandaa ratiba maalumu itakayojumuisha
shughuli zako zote za kila siku kama ilivyokua kipindi upo chuoni. Kwa mfano
kama ulikua unahudhuria mazoezi ya jioni kila siku baada ya masomo yako basi ni
vivyo ivyo hata baada ya kumaliza masomo hakikisha unapotoka kwenye harakati
zako za kila siku unaenda mazoezini kama siku zote.
USIWE NA SHAKA HATA KAMA HUJAPATA KAZI UNAYOITAMANI KATIKA
MAISHA YAKO (DREAM JOB)
Hata kama si kazi yenye kukidhi mahitaji yako ya kila siku,
usikatae kufanya kazi! Fanya kwa muda wakati uinaendelea na michakato mengine
ya kutimiza ndoto zako. Kupata kazi moja kunafungua mianya ya kupata kazi
nyingine. NUKUU YA USEMI WA WAHENGA “MTEMBEA BURE SIO SAWA NA MKAA BURE” kwa
hili suala ata wewe huna budi kuwaunga mkono wahenga.
FAIDIKA NA RASILIMALI ZILIZOKUZUNGUKA
Licha ya maisha yetu ya kawaida ya kuzunguka sehemu mbalimbali.
Hakikisha unazijua rasilimali zote unazopaswa kua nazo kwa kipindi icho kama
mfanyakanzi katika kampuni husika. Usiogope kuuliza! (Kwani kuuliza si ujinga)
Ukiwa kama mfanyakazi mpya unapaswa kuwa karibu na boss pamoja na wafanyakazi
wenzako ili kuweza kupata taarifa zaidi juu ya masuala muhimu kufanikisha
utendaji wako wa kazi.
Kwa mfano: upatikanaji wa chanzo cha mtandao (internet) na
bima mbalimbali.
Ulikua unaishi kwa tsh 10,000 kwa siku, hakikisha hauvuki
kiwango kuzidi kipato chako cha siku cha kawaida. Na kama inawezekana
nakushauri udumu katika kiwango ichoicho kwa muda flani mpaka pale vyanzo vya
kipato vinapoongezeka. Lipa madeni,
endelea kuhifadhi fedha. Na kama unatumia kuzidi kipato chako, una hatari
ya kutumbukia kwenye utumwa wa ajira kwa kipindi kirefu.
"Mtanzania wa kawaida anayeweza kumudu kupata tsh 5000 kwa
siku. Akifanya matumizi ya tsh 4000 na kuweka akiba tsh 1000 kila siku.
Ni makadilio ya kuvuna tsh 365,000 kila mwisho wa mwaka.
1,825,000 ndani ya miaka mitano".
Je? Vp wewe msomi wa chuo kikuu uliyeibeba shahada ya kwanza
ya sheria, ualimu, afisa masoko, afisa ugazi, afisa rasilimali watu au
udaktari. Mwenye makadirio ya kuweza kumudu kupata tsh 10,000 kwa siku.
Hifadhi japo tsh 5000 tu kwa siku ili baadae ikuzalishie
1,825,000 ndani ya mwaka mmoja.
Makadirio ya kuvuna tsh 9,125,000 baada ya miaka mitano.
Hesabu hizi ni nje ya mshahara, vijibiashara vidogo vidogo
na vyanzo vingine vinavyokuingizia kipato.
Msingi imara wa kudumu katika utendaji, ni kuipa thamani
kazi uliyoipata. Tambua ,manufaa yake ata kama ni kidogo kulingana na gharama
za maisha zinazopanda kila kukicha. Jenga mawazo chanya, fanya kazi kwa muda
husika, tengeneza mazingira rafiki ya kazi na hakikisha unajenga mahusiano
mazuri na wafanyakazi wenzako. Ukizingatia haya nakuhakikishia mwanzo mzuri wa
safari yako kuelekea kwenye kilele cha mafanikio.
Suala la msingi zaidi ni afya tukizingatia afya ni uhai.
Hakikisha unapata milo mitatu kila siku, kula vyakula vyenye virutubisho vya
kujenga mwili na kuupa kinga dhidi ya magonjwa. Sambamba na matunda pia maji ya
kutosha wakati wote. Mazoezi ni tatizo kubwa linalowakabili asilimia kubwa ya
watanzania. Tukiwa na Imani ya kua mazooezi ni kwa ajili ya wana michezo tu!
Mazoezi yatakufanya ujisikie mwepesi na mwenye afya tele usiye sumbuliwa na
magonjwa madogomadogo.
JIFUNZE MAMBO MAPYA UNAPOPATA FURSA ZA KUSAFIRI SEHEMU
MBALIMBALI.
Unaposafiri katika maeneo mapya hakikisha unaitumia vizuri
fursa iyo kujifunza. Tembelea nyumba za makumbusho, mbuga kama zipo, soko,
kanisa na misikiti. Jifunze tamaduni na desturi zao, namna jamii iyo
inavyoendesha maisha yake ya kila siku. Na pia ijue mitaa yote iliyokaribu na
unayoweza kumudu kuitembelea.
Jitambue!
Sual la mwisho la msingi ni kutambua ya kwamba muda nliokua
naupoteza chuo, kwa hivi sasa una thamani ya hali juu kuikamilisha safari hii.
Chuoni tulipata muda mwingi wa kuzurula na marafiki, kupika, kufua nk. Wengi
wetu tulikua hatujui kama muda wa kufua au kupika unaweza ukawa na thamani
mfano wa fedha tunayoitafuta. Nukuu kutoka kwa mwandishi.
MFANO:
DAKIKA MOJA INAWEZA KUWA NA THAMANI YA TSH 100 TU!
DAKIKA 60 ( SAA MOJA) IKIWA NI SAWA NA THAMANI YA TSH 6,000
DAKIKA 1440 ( MASAA 24)siku moja THAMANI YA TSH 144,000
Kwa makadirio haya wengi wetu tutatahamaki na kushika midomo
baada ya kugundua tumeshapoteza mabilioni ya fedha tangu kujitambua kwetu. MUDA
NI PESA! OKOA MUDA! TUNZA MUDA!
No comments:
Post a Comment