Friday, 21 August 2015

MBINU BORA ZA KUHIFADHI NA KUTUMIA MUDA KIUZALISHAJI_(TIME MANAGEMENT) MUDA NI PESA_gpangetz.blogspot.com

“Kuwa na ufahamu juu ya matumizi sahihi ya muda, Itakupa morali ya kuutumia muda wako mwingi katika shughuli za uzalishaji zitakazokuongezea kipato.
Sina uzoefu wa kusoma sana vitabu japo sichoki kuthubutu, kutohoa mawazo chanya kwenye kila kitabu kitakachopita mikononi mwangu. 7 Habits of Highly Effective People by Stephen Covey. Ni moja ya vitabu vikongwe kabisa kilichomudu katika ubora wake kwa kipindi kirefu. Ukurasa wenye mada juu ya matumizi sahihi ya muda umetafsiri baadhi ya shughuli zilizotuzunguka wengi miongoni mwetu na kuzigawa katika makundi manne (4). Na Ukweli wa mada hii, ndani yake una makundi mawili ya shughuli za kila siku
1. SHUGHULI MUHIMU.                                                                    
2. SHUGHULI ZENYE UHARAKA.

    
Ufanyaji wa shuguli hizi kwa kipindi tofauti huleta mchanganuo wa makundi manne haya.
 Zingatia: kwa muongozo huu utaweza kufanya maamuzi sahihi na kuelekeza muda wako mwingi kwenye shughuli za uzalishaji.
Kwanza lazima wote tuelewe nini maana ya maneno haya mawili, shughuli muhimu na shughuli zenye uharaka.
·        Muhimu inawakilisha thamani ya shughuli husika. Mfano mzuri ni maandalizi ya taarifa ya utafiti (research)
·        Uharaka ikiwa na maana ya ukamilishaji wa shughuli husika mapema iwezekanavyo. Kwa mfano, Kutatua maulizo ya mteja.


Tatizo ni pale tunapojikuta tunatumia muda wetu mwingi katika shughuli zenye uharaka Zaidi yaani A na C na kusahau shughuli B na D. Mara nyingine kuzitupilia mbali pasi kufikiria. Watu wanaoshi kwenye misingi ya uharaka daima wanajivunia kuwahi kumaliza shughuli zao pasipo kujali wala kuzingatia kukua kiuchumi. Kwa masikitiko makubwa wanajikuta wanateseka katika maeneo yao ya kazi na maisha kwa ujumla. Wengi wetu tumeshawahi kuzisikia hadithi na mifano mingi ya watu wa aina hii.
Maeneo ya jirani na ninapoishi kuna wafanyabiashara wenye matamanio ya kufanya mauzo ya hali juu lakini hawawezi na hawajawahi kutenga muda kwa ajili ya kwenda kwenye mafunzo ya kuzijua mbinu za kibiashara. Wanatumia muda wao mwingi shughuli zisizo na thamani, shughuli za uharaka, zisizo na umuhimu kama vile kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii na kuangalia televisheni.
Wameegemea kwenye masuala yasiyo na msingi. Sina maana kwamba kuperuzi na kutazama luninga si masuala ya msingi ila kama zinagharimu ujenzi wa maisha na afya yako kwa ujumla, basi sio masuala sahihi kwa kipindi hicho.

SWALI:
NINI CHANZO CHA MATOKEO HAYA?
 MAJIBU
Ni Kwasababu shughuli za kipengele (B)
·        Ni lazima ziwe na mpangilio na nidhamu katika ufanyikaji wake. Haziwezi kutokeo tu pasipo kupangiliwa kama jinsi shughuli za uharaka zinavyojitafsiri. Je? Kama hutafanya siku ya leo itakuathiri nini! HAZIWEZI KUTOA UHAI WAKO! Kwa mfano kama hutapoteza muda wako kufanya maongezi yasiyo na tija kila wakati, je? Itakuathiri vipi kitaaluma na katika harakati zako za utafutaji. HIZINA ULAZIMA!
FANYA JARIBIO HILI
TEGESHA MLIO (alarm) KILA BAADA YA NUSU SAA KATIKA SIMU YAKO YA KIGANJANI. KISHA ORODHESHA SHUGHULI ZOTE ULIZOZIFANYA NUSU SAA IYO ILIYOPITA. FANYA HIVI KWA MUDA WA SIKU TATU (3).
 Nina amini utapata mshituko mkubwa sana baada ya kugundua unatumia muda mwingi sana kwenye shughuli za kipengele (c) na (d) zisizo na tija wala umuhimu katika kukuza kipato na maisha yako kwa ujumla.
Kwa hili nina uwakika kabisa utatamani muda uongezeke katika kufanya shughuli za kipengele (A) na (B). Habari njema ni kwamba, baada ya kufanya hili jaribio itakupelekea kuongeza upeo na umakini mkubwa katika matumizi yako ya muda.
Watu makini katika maisha ni wale waliobobea katika taaluma ya utunzaji muda na mpka kushawishi wengine kufuata nyayo zao. TUMIA SOMO HILI IPASAVYO ILI UWE MMOJA YA MIFANO YA KUIGWA KATIKA JAMII YAKO.








2 comments:

  1. Hizi namba ni kwa ajili ya nini Nakupigia jamaa unaniweka loud speaker then un kata simu ukijitoa kwa jamii jitoe kwa kusaidia watu hustake sifa tu
    Jirekebishe ukipigiwa simu msikilize mtu ana nin umenionesha dharau sana mshikaji

    ReplyDelete
  2. mwenye hii namba jirekebishe +2550763899645

    ReplyDelete